Saturday, March 10, 2012

MACHO YETU YAMTAZAME BWANA KWA AJILI YA TANZANIA

Wapendwa tunaishi katika kipindi chenye hofu nyingi.Hivi karibuni nchi yetu imeingia katika aina mbalimbali za migomo. Lililo zito zaidi ni mgomo wa madaktari.Yanasemwa mengi.Hatujui undani zaidi wa jambo hili.Serikali ina maelezo yake na madaktari wana maelezo yao.Sisi raia wa kawaida kwetu ni kitendawili kwa sababu kila upande unatushawishi kukubali maelezo yao. Ushauri wangu kwa kila mtu mwenye hofu ya Mungu ni huu;tuwapeleke madaktari na serikali madhabahuni pa Mungu atuamulie.Macho yetu yamtazame Bwana katika hili.Mbarikiwe.Mungu ibariki Tanzania.

2 comments:

  1. Amina baba mhungaji. MUNGU mwenye nguvu azidi kukuwezesha na kukuinua siku hadi siku. Nabarikiwa sana na wewe mtumishi.

    ReplyDelete
  2. Asante sana Tamilwai kwa kupitia moyo. Mungu akubariki sana na endelea kuniombea kwa uaminifu

    ReplyDelete